Mfuko wa Ebola waahidiwa Afrika


Ebola

Wafanyabiashara na makampuni mashuhuri ya Afrika wameanzisha mfuko wa dharura kusaidia nchi zilizoathirika na Ebola.
Mkutano wa mwanzo wa kuahidi msaada uliofanywa Addis Ababa, Ethiopia, umekusanya dola milioni 28.5.
Fedha hizo zitatumiwa kutuma wafanya kazi wa utibabu 1,000 kwenda Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Benki ya maendeleo ya Afrika itasimamia mfuko huo.
Hatua hiyo ni sehemu ya msaada wa Umoja wa Afrika kwa nchi zilizoatthirika.
Akizungumza baada ya mkutano huo, mwenyekiti wa AU, Dlamini Zuma, alisema fedha zitazopatikana ni sehemu ya mradi wa muda mrefu wa kupambana na majanga kama hayo siku za mbele.
Na makampuni yanayotoa huduma kwa simu za mkononi za Afrika yamesema kuwa mwezi ujao yataanzisha kampeni ya kuwapa nafasi wateja wao kusaidia nchi zenye Ebola, kwa kutoa mchango kwa kutumia ujumbe wa simu, SMS.
Inaarifiwa kuwa Afrika ina wateja milioni 700 wa simu za mkononi.
Ijumaa, shirika la madaktari la kimataifa, MSF, lilisema idadi ya wagonjwa wepya nchini Liberia inapungua.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment