Kwa
mara nyingine Chelsea imeonyesha ni moto wa kuotea mbali baada ya
kuifunga Liverpool 2 - 1 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa
Anfield.
Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli
lililotiwa wavuni na Emre Can baada ya kupiga shuti na kumgonga beki
mmoja wa Chelsea na kujaa wavuni.Baadae Chelsea wakaja juu na kusawazisha goli kupitia kwa Gary Cahill baada ya mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet kuingia na mpira wavuni wakati alipokuwa ameudaka. Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa kwa shuti kali umbali wa takribani meta 15 ndani kisanduku cha 18.
Mechi hiyo ya Chelsea na Liverpool katika uwanja Anfiled kunarejesha kumbukumbu zisizofurahisha kwa upande wa Liverpool pamoja na hali yao ya baadaye ambayo si nzuri sana.
Awali katika msimu uliopita mwishoni mwa mwezi Aprili ,kombe la ligi hiyo lilionekana likitaka kuelekea Liverpool lakini baadae ndoto hiyo ilifutika kabisa.
Diego Coast alieanza katika mechi dhidi ya Liverpool bado anaonekana ni moto wa kuotea mbali hasa kwa bahati yake ya kufunga magoli.
Mchezaji huyo wa Uhispania awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la paja na aliorodheshwa katika kikosi dhidi ya Maribor katikati ya wili lakini hakucheza.
0 maoni:
Post a Comment