Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata
ya Matui Wilayani Kiteto Bw. Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara
wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na
wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa
vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw. Eliakimu Ndelekwa.(Picha na
Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na wananchi wa
Kata ya Matui Wilayani Kiteto wakati alipofanya ziara wilayani humo
kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji
iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na Mtendaji wa
Kijiji cha Chekanao, Kata ya Kiperesa, wilayani Kiteto Bw. Omar Ndee
(kulia) wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa
migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea
mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo. Katikati ni Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimike pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho
Bw. Japhet Chafu (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kiteto
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameahidi kuongeza idadi ya
Askari katika kijiji cha Chekanao, kata ya Kiperesa wilayani Kiteto
Mkoani Manyara kufuatia wananchi katika kijiji hicho kujitolea nyumba
kwa ajili ya kuishi Askari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo
yao kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi inayosababisha kutokea kwa
mauaji.
IGP
Mangu aliyasema hayo jana wakati alipokuwa katika ziara Wilayani Kiteto
ya kujionea uharibifu uliojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wa
migogoro hiyo iliyopelekea kutokea kwa vifo vya wakulima na wafugaji
hivi karibuni katika wilaya hiyo ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi kutokana na vurugu hizo.
Alisema
kufuatia kuwepo kwa umbali mrefu wa kituo cha Polisi na kijiji hicho
atahakikisha askari wa kudumu wanakuwepo ili kushirikiana na wananchi
katika kuwabaini wahalifu wanaofanya vurugu na kuendeleza migogoro hiyo
ambapo wananchi nao waliahidi kujenga kituo cha Polisi.
Kwa
upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao Bw.Omar Ndee alisema
wamekuwa wakipata shida kutokana na umbali mrefu wa kituo cha Polisi
jambo ambalo limekuwa likifanya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu
vinavyochangiwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Japhet Chafu alilishukuru Jeshi la Polisi
kwa kuimarisha usalama kijijini hapo tangu kutokea kwa mauji ya wakulima
na wafungaji ambapo alibainisha kuwa bila kuwepo wao hali ingekuwa
mbaya zaidi kutokana na kutokuwepo na muafaka baina ya wakulima na
wafugaji.
“IGP
hawa askari wako wasingekuwepo hapa usingekuta mtu lakini tunawashukuru
sana hawa askari kwa kuwa hivi sasa hali ya usalama imerejea na hata
shambani tumeanza kwenda” Alisema Bw.Chafu.
IGP
Ernest Mangu alitumia ziara hiyo kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya
Kiteto, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakaguzi wa Tarafa pamoja
na Askari Kata ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuimarisha
hali ya ulinzi na usalama.
0 maoni:
Post a Comment