Katibu CCM wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu akikagua wachezaji kabla ya mchezo kuanza
Mtaturu alionyesha umahiri wa kupiga penati kuashiria kufunguliwa kwa mashindano hayo
Viongozi mbalimbali wa CCM Mufindi wakifuatilia mtanange huo wakati wa ufunguzi.Picha zote na (Mathias Canal)
Yohanes Kaguo, Diwani kata ya Makungu akizungumzia mashindano hayo
Diwani Kaguo akikagua wachezaji kabla ya mechezo kuanza
Mtaturu akinena jambo kabla ya mchezo kuanza
Na Mathias Canal-Mufindi
Mashindano
ya mpira wa miguu yanayojulikana kama Kaguo Cup 2014 yameanza rasmi
Wilayani Mufindi ambapo yatazikutanisha timu nane kutoka vijiji tofauti
tofauti Wilayani humo.
Akizungumza
na vijana waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Diwani wa
Kata ya Makungu, Yohanes Kaguo alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni
kuwaweka vijana pamoja ili kuimarisha mahusiano mazuri baina yao ikiwa
ni pamoja na kuwahamasisha kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la
mkazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kaguo
aliongeza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 13/12/2014
siku moja kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo kupitia
mashindano hayo vijana watakuwa wamehamasika kujihusisha na shughuli za
maendeleo ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji sambamba na kujiadhikisha
na kupiga kura.
kwa
upande wake Meshack Luhala ambaye ni katibu wa kamati ya michezo hiyo
alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu 8 ambapo katika kundi A
kutakuwa ni timu nne na kundi B vivyo hivyo kutakuwa na timu nne.
Alizitaja
timu hizo kuwa ni Kitasengwa Fc, Lugema Fc, Super Star Fc, Villa Fc,
Mpm Fc, Lugolofu Fc, Watumishi Fc pamoja na G.R.L Fc.
Aliongeza
kuwa katika mashindano hayo mshindi anatarajia kujinyakulia kikombe
pamoja na kitita cha shilingi 500,000, Mshindi wa pili atajinyakulia
shilingi 300,000 huku mshindi wa tatu akijinyakulia shilingi 200,000
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo, Miraji
Mtaturu ambaye ni katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi
alisema kuwa kila kijana anapaswa kujihusisha kwenye michezo ili
kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, ngono zembe sawia na wizi.
Alisema
kuwa mashindano hayo yameanzishwa maalum kwa ajili ya vijana ili
kuhamashisha amani, Upendo na mshikamano uendelee kudumu Wilayani humo.
"Leo
ninayafungua mashindano haya ya mpira wa miguu lakini kila timu
inayocheza leo kwenye ufunguzi huu, nitaipatia shilingi 50,000 pia ili
kusukuma mashindano haya Ofisi yangu CCM Wilaya itachangia shilingi
200,000 ambazo nitamkabidhi Diwani wenu" Alisema Mtaturu
Mtaturu
alisema kuwa kila mchezaji anapaswa kuweka nia ya kufanya vizuri ili
aweze kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara kwani kucheza bila malengo na
kujituma itafanya vijana wasipate ajira kwenye timu mbalimbali duniani
kote.
Aidha
kauli mbiu ya mashindano ya Kaguo Cup 2014 "VIJANA KUJIEPUSHA NA UKIMWI"
inatarajiwa kuwafikia vijana wengi hivyo kuhamasika kupima na kufanya
mapenzi salama kwa kutumia kondomu ikiwa ni njia sahihi ya kujikinga na
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi/Ukimwi.
Hata
hivyo mashabiki waliojitokeza kwenye mashindano hayo walishuhudia mchezo
huo kati ya Lugema Fc na Villa Fc ukimalizika kwa timu zote kuchoshana
nguvu kwa kufungana goli moja kwa moja ambapo timu ya Lugema Fc ndio
ilikuwa ya kwanza kupata goli la kuangoza katika dakika 66 kupitia kwa
mshambuliaji wake Bakari Mwalimu kabla ya Fred Kipondamali kuisawazishia
timu Villa Fc katika dakika 72 ya mchezo hivyo kupelekea mashindano
hayo kumalizika kwa sare.
0 maoni:
Post a Comment