Kwa
mara ya pili katika kipindi cha juma moja ,kikao cha wabunge wa Somali
kilichoitishwa ili kuijadili hatma ya waziri mkuu nchini humo kimeisha
kwa kelele na ghasia.
Wabunge walitarajiwa kupiga kura ya kutokuwa
na imani na waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed ,lakini wafuasi wake
walikataa kukaa na kuanza kuimba na kubeba mabango.Bunge la Somali limelemazwa na mgogoro uliopo kati ya waziri mkuu na rais Hassan Sheikh Mhamud.
Marekani imesema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haina maslahi ya raia.
Umoja wa mataifa nao umesema kuwa una wasiwasi kuhusu ufisadi wa ununuzi wa kura unaokabili kura hiyo.
0 maoni:
Post a Comment