Kuhusu huduma ya kutumiana taarifa


Huduma ya kushirikisha taarifa ni nini?
Huduma hii inakuruhusu kuchangiana taarifa kutoka BBC kupitia kwa mfumo wa runununa watu kupitia kwa barua pepe na mitandao ya kijamii.
Unawezaje kumtumia mwenzako taarifa kwa Barua pepe?
Huduma hii inakuwezesha kuchangiana taarifa za BBC kwenye mtindo wa Rununu kupitia barua pepe kwenye simu yako ya mkononi.
Huduma hii inatumika vipi?
Ukiona taarifa za BBC kwenye mtindo wa Rununu ambayo unataka kumtumia mwenzako, bonyeza kwenye alama ya barua pepe katika sehemu ya kuchangiana taarifa mwishoni mwa ukurasa. Sehemu ya barua pepe itafunguka mara moja kwenye simu yako, ili uweze kupata anwani ya mtu unayetaka kumtumia taarifa hiyo , kisha andika ujumbe kuhusu taarifa hiyo unayotaka kumtumia mwenzako.
Kwa nini sijafanikiwa kutuma taarifa?
Utahitaji huduma ya kukuwezesha kutuma barua pepe kwenye simu yako ili uweze kuchangiana taarifa za BBC kwa mfumo huu. Ikiwa una shaka kuhusu namna ya kutumia huduma ya barua pepe kwenye simu yako, fuata maagizo kuhusu namna ya kutumia simu yako.
Huduma hii itakugharimu nini?
BBC haitakutoza chochote kutumia huduma hii ya kuchangiana taarifa kwa barua pepe. Hata hivyo kampuni ya huduma ya simu unayotumia inaweza kukutoza kiwango kidogo cha pesa kwa data utakayotuma. Ikiwa haujui kiwango cha pesa kinachotozwa kwa kiasi Fulani cha data, tafadhali uliza mtandao wako wa simu.
Je BBC inahifadhi taarifa zangu za siri?
Hapana. Kwa kuwa utakuwa unatumia barua pepe yako hatuwezi kupatadata yako ya faragha au hata ujumbe wako. Soma zaidi kuhusu sera ya faragha ya BBC
Je huduma hii ya kuwatumia wenzako taarifa inatumika vipi kwa Facebook, Twitter au mitandao mingine ya kijamii?
Inakuwezesha kutumiana taarifa kutoka kwa mtindo wa BBC wa Rununu kupitia ukurasa wako wa Facebook, Twitter na hata mitandao mingine ya kijamii.
Inatumika vipi?
Ukiona ukurasa wa BBC unaotumia mtindo wa rununu, bonyeza kwenye kiashiria cha Facebook au Twitter katika sehemu ya kuchangiana taarifa mwishoni mwa ukurasa huo.
Kisha ukurasa wa Facebook au Twitter utajitokeza au hata mtandao wa kijamii unaoutaka, ili uweze kuingia kwenye akaunti yako. Utaweza kuongeza ujumbe . Ikiwa unachangia taarifa kupitia kwa Twitter au google+, picha itatumwa kutoka kwa ukurasa huo pia.Ukarasa unaotaka kumtumia mwenzako, utaonekana kwenye ukurasa wako wa Facebook au Twitter .
Je ni lazima niwasilishe data yangu ya faragha kwenye Facebook au Twitter kwa BBC?
Hapana. Unapobonyeza kwenye kiashiria cha BBC au Twitter, utahamishwa kutoka katika ukurasa wa Mobile wa BBC hadi katika ukurasa wako wa Facebook au Twitter , kwa hivyo BBC haina uwezo wa kupata data yako ya faragha hata kidogo.
Kwa nini siulizwi taarifa zangu za faragha?
Katika baadhi ya simu za mkononi, taarifa zako za siri huhifadhiwa na Faebook au Twitter, maana kuwa sio lazima uingie upya kila mara kwenye akaunti yako.
Je BBC inahifadhi data yangu ?
Hapana. Kwa kuwa utaondoka kwenye ukurasa wa BBC na kuingia kwenye akaunti yako, hatuwezi kupata taarifa zozote za faragha kwenye ukurasa wako wa Facebook. Kwa taarifa zaidi kuhusu sera ya BBC kuhusu data ya faragha ya watu, tafadhali soma sera hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment