Mwakalebela akikabidhi vifaa vya muziki kwa viongozi wa CCM Iringa mjini
Na Mathias Canal, Iringa
Mjumbe wa mkutano mkuu (CCM) Taifa ambaye pia ni kamanda wa umoja wa vijana Iringa mjini, Frederick Mwakalebela, ametoa vifaa vya mziki kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Iringa Mjini, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba Mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, alisema kuwa CCM ina kazi kubwa ya kuhakikisha inapata ushindi wa kishindo katika uongozi wa serikali za mitaa hivyo moja ya nyenzo muhimu ya ushindi wa chama hicho ni kuweza kuhamasisha wananchi kwa vichocheo vya vifaa hivyo vya muziki.
"Nina imani utawekwa utaratibu mzuri ambao utawezesha viongozi wote kutumia vifaa hivyo wakati wa kampeni katika Kata zote, na leo nimekabidhi risiti ya vifaa vyote ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 8.1" Alisema Mwakalebela
Aliamua kutoa vifaa hivyo kutokana na gharama nyingi ambazo chama hicho kimekuwa kikitumia wakati wa mikutano yake hivyo ili kuepukana na gharama hizo aliona ni bora kukisaidia chama hicho.
Mwakalebela alisema kuwa anatarajia kutoa mchango wake kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa maabara huku akiahidi kuunga mkono juhudi na shughuli za aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dkt Christine Ishengoma
Mwakalebela ambaye aliwahi kuwa mfadhili mkubwa wa timu ya polisi Iirnga kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa LIpuli alisema kuwa anashiriki katika kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja na hatimaye kupanda ligi kuu.
Alisema ametafuta vijana wa kushangilia na kuleta hamasa ya ushindani wakati timu hiyo inapocheza mechi zake Jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Post a Comment