Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amewafukuza kazi ama kuwastaafisha mapema maafisa wa jeshi Zaidi ya 30.
Hakuna majina yaliyotangazwa, lakini imeanza kuripotiwa mjini Baghdad kwamba kati ya hao walioondolewa anaweza kuwemo mkuu wa majeshi.
Katika taarifa yake Bwana Abadi amesema amechukua uamuzi huo kuweza kuliimarisha jeshi Zaidi na kuwa lenye weledi pamoja na kupambana na rushwa.
Mwandishi wa BBC anasema kuondoshwa kwa wanajeshi hao ni matokeo ya kushindwa kupambana na wanamgambo wa kundi la Islamic State, wakati walipofanya mashambulio kaskazini mwa Iraq mwezi June.
0 maoni:
Post a Comment