MAKINDA RAIS BUNGE LA SADC


Anne Makinda
Wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Bunge la nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini (SADC PF) wamemchagua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, kuwa Rais wa Bunge hilo miaka miwili ijayo.

Makinda ambaye hakuwa na mpinzani, aliungwa mkono na wajumbe wote wa Mkutano huo ambao uliomalizika juzi.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC, Dk. Esau Chiviya, alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za Bunge hilo, kanuni ya Kanuni ya 42 (2) i  inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee, basi  atawahoji wajumbe na kama watamkubali basi atamtangaza rasmi kuwa amechaguliwa.
“Kwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, hana mpinzani na kwa kuwa nimewahoji na wote mmemuunga mkono, basi natangaza kuwa ndiye Rais mpya wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo,” alisema Dk. Chiviya.
Awali kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi ndani ya chombo hicho, Makinda alitakiwa kugombea nafasi hiyo pamoja na Spika wa Ushelisheli na Msumbiji ambao waliamua kuamua kumuunga mkono Makinda.
“Ninalo deni kubwa kwenu kwa jinsi mlivyoniunga mkono na kama mnavyojua jukumu letu kubwa mbele yetu ni kuwa na Bunge imara la SADC jambo ambalo nawahakikishia kwa pamoja tutafanikiwa,” alisema Makinda katika hotuba ya kushukuru.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment