Moja ya mashua ikisukumwa kurejeshwa katika eneo lake la hifadhi baada ya kumaliza mashindano hayo.
Na Mwandishi Wetu
MICHUANO
ya siku 2 mwaka ya waendesha mashua za kisasa kuwania kombe la Mercedes
Benz kwa mwaka huu imemalizika juzi jioni kwa waendesha mashua Al Bush
akisaidia na Pugwash wakitwaa ushindi wa jumla na kutwaa kombe la
Mercedes Benz.
Waendesha
mashua hao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba
2653 wakikabidhiwa kombe hilo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO,
Wayne McIntosh ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini
Tanzania.
Akizungumzia
mashindano hayo Mratibu wa waendesha mashua hao Michael Sulzar alisema
yalikuwa na ushindani mkubwa na kwamba ingawa siku ya kwanza bahari
ilikuwa shwari siku ya pili bahari ilikuwa chafu na kufanya wenye
mashua kuwa na kazi ya ziada.
Alisema
kwa kawaida mchezo huo unakuwa mtamu pale ambapo bahari inakuwa ‘ngumu’
ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye
mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti.
Mratibu
wa waendesha mashua Michael Sulzar akitangaza matokeo ya mashindano ya
kuwania kombe la Mercedes Benz 2014 yaliyofanyika katikati ya wiki.
Jumla ya timu kumi na nne (Mashua) zilishiriki katika michuano hiyo ya
siku mbili.
Pamoja
na washindi hao wa jumla ambao walikuwa katika mashua ya kisasa zaidi
yenye Tanga mithili ya baluni washindi wengine ni Tony Hughes na
Richard Stanley wakiendesha mashua Popo bawa yenye namba 2648 aina ya
Hobie Tiger.
Mshindi wa tatu alikuwa Cyrille Girardin akiwa na Olivier Praz waliokuwa na mashua ya Theluji namba 72 aina ya Hobie 16.
Michael
Sulzer na Andreas Schimidt wao walipata tuzo ya wawili waliofanya
vyema. Wawili hao walikuwa katika mashua Die Wilde 13 yenye namba 1659
aina ya Nacra Infusion.
Aliyetwaa tuzo ya uanamichezo bora ni Mark Henderson na Shane Rumbold waliokuwa katika mashua Shark aina ya Hobie tiger.
Waendesha
mashua Al Bush na mwenzake Pugwash wakiwa na kombe la ushindi la
Mashindano ya mashua ya siku mbili ya kombe la Mercedes Benz
yaliyofanyika jijini Dar es salaam Yatch Club.Washindi hao walikuwa
wakiendesha mashua yao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa
na namba 2653.Walikabidhiwa kombe hilo hivi karibuni na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh (kulia) ambao ndio
mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.Wa Pili kulia ni Meneja
Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.
Mshindi
wa kwanza katika mashua za kawaida alikuwa David Scott akiwa na
Christina waliokuwa na mahsua Alphacrucis yenye namba112483 aina ya
Hobie16. Mshindi wa pili wenye mashua Polo aina ya Hobie 16 yenye namba
111206 Andrew Boyd na Kim Troll.
Mshindi wa tatu alikuwa Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren
waliokuwa katika mashua namba 2657 aina ya Hobie Tiger iliyojulikana
kama 1.
Jumla ya Mashua 14 zilishindana katika michezo iliyoandaliwa katika klabu ya Yatch ya Dare s salaam Msasani.
Baada
ya shamrashamra za kupeana vikombe na tuzo nyingine Ofisa Mtendaji Mkuu
wa CFAO Motors, Wayne McIntosh alipata nafasi ya kuzungumzia michuano
hiyo ambayo imekuwa ikidhaminiwa na Mercedes Benz kwa miaka zaidi ya
sita sasa.
Mtoto
wa mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida David Scott (ambaye
aliendesha mashua hiyo akiwa na Christina) akimsalimia Ofisa Mtendaji
mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh kabla ya kukabidhiwa tuzo ya wazazi
wake ya ushindi.
Mark Henderson na Shane Rumbold wakikabidhiwa tuzo ya uanamichezo bora, walikuwa katika Mashua Shark aina ya Hobie Tiger.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh akizungumza kabla ya
kukabidhi kombe la Mercedes Benz kwa washindi wa jumla Al Bush na
mwenzake Pugwash. Michuano hiyo ilianzia na kumalizikia Dar Yatch Club
Msasani. Kulia aliyebeba kombe hilo ni Meneja Masoko wa CFAO Motors,
Tharaia Ahmed.
0 maoni:
Post a Comment