MWANAMKE AJITOA MUHANGA CHUONI NIGERIA

Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa kero kwa serikali na wananchi wa Nigeria
Mwanamke mmoja amejilipua katika chuo cha mafunzo Kaskazini mwa Nigeria.

Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa bomu lililipuka huku mwanamke huyo akijiandaa kuingia katika ukumbi uliokuwa umejaa wanafunzi mjini Kontagora.
Idadi ya majeruhi bado haijulikani , lakini mwalimu mmoja alimbia BBC kuwa aliona miili minne ikiwa katika hali mbaya.
Wapiganaji wa Kiisilamu Boko Haram wanaendesha harakati za kivita dhidi ya serikali ya Nigeria, harakati ambazo zimekuwa zikiendelea kwa miaka mitano iliyopita.
Kundi la Boko Haram, limeyatangaza kuwa dola za kiisilamu baadhi ya majimbo wanayoyadhibiti, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kadhalika kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi na mauaji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria tangu kuanzisha harakati zake mwaka 2009.
Watu wanasema walisikia mlio mikubwa kabla ya watu kuanza kukimbilia usalama wao.
Wanajeshi walikimbia kwa harakan katika kituo hicho baada ya shambulizi na hata kuziba eneo zima.
Tatu kati ya miili minne iliyoonekana ilikuwa ya wanawake.
Baadhi ya walioshuhudia shambulizi hilo walisema kuwa mwanamke aliyekuwa amejifunga mabomu hayo pia aliuawa.
Takriban watu 7 walijeruhiwa vibaya ingawa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment