Baba
mtakatifu Francis ametaka milango ya majadiliano na kundi la wanamgambo
wa dola ya kiislam iwe wazi ,ingawa hali ni mbaya na ya kutatiza katika
maeneo wanako tekeleza mashambulio yao.
Papa
Francis ameyasema hayo wakati akirejea mjini Rome, Italia,baada ya
kulitembelea bunge la muungano wa jumuiya ya Ulaya lilifanyika katika
mji wa Strasbourg, Papa pia amesisitiza makubaliano ya kimataifa
kutokomeza ugaidi yalikuwa muhimu.na hakuna ulazima wa nchi kupigana na
ugaidi ikiwa peke yake nguvu ya pamoja ni muhimu sana.
Akilihutubia
bunge hilo ,alishusha mvua za lawama kwa muungano huo kuwa una hatia
kwa kuweka sheria zilizokuwa kali na za kuumiza, hasa katika suala la
wahamiaji na kuonya kuwa Mediterranean isifanywe kuwa kaburi la
wahamiaji wanaosafiri kwa boti kutokea upande wa kaskazini mwa Africa.CHANZO:BBC
0 maoni:
Post a Comment