Neno la Wakati Mwema
Ndugu Zangu nilipata nafasi ya kufika Kijiji cha Utosi kilichopo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa kwa muktadha wa kujua tatizo lililopelekea wananchi wa kitongoji cha Mbugi kugomea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Watu hawa walikuwa wakilalamikia swala hilo kutokana na ahadi ya mkuu
wa Wilaya ya Mufindi pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo waliyoitoa ya
kuhakikisha kijiji kinapatikana lakini hakijapatikana na mgogoro huo
umedumu takribani miaka minne sasa.
Nikiwa kijijini hapo nilipata nafasi ya kuzungumza na wananchi hao lakini walishangaa nilipopinga kukaa kwenye kiti cha plastiki na kuomba kukaa kwenye kigoda alichokalia Bibi mmoja ambaye nilihisi anapata mateso na kumuachie yeye ndiye akae kwenye kiti cha plastiki.
Nilipomaliza kufanya mahojiano na watu hao hakika nilitafakari juu ya Kigoda cha Mwalimu lakini katika tafakuri yangu nikasema ndani ya nafsi Hivi kumbe si kila Kigoda ni cha Mwalimu na kama ni cha Mwalimu mbona kipo Kijijini Utosi.
Naam si kila litamkwalo linabeba ujumbe wa wazi mengine hubeba ujumbe mficho, Loooh kumbe Kigoda cha Mwalimu sio kigoda cha yule bibi kijijini Utosi bali ni msemo uliotumiwa kitaasisi.
Ni neno la Wakati Mwema
Salaaam
Mathias canal

0 maoni:
Post a Comment