Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma
za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro (wa tatu kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo,wakati akitoa wito wa kujiondoa ubia kwa Kampuni ya Bhart Airtel
katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kutoka kulia ni Mfanyakazi wa
Tewuta, Rashid Rajab, Mwanasheria Beatrice Monyo, Mwenyekiti Taifa wa
Tewuta, Pius Makuke, Mwanasheria, Leila Farijalah na Ofisa wa Masijala,
Ericla Frank.
Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wameitaka Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Bhart Airtel kujitoa ubia ndani ya TTCL.
Mwito huo umetolewa na Katibu Mkuu
wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za
Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro kwa niaba ya wenzake wakati
akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi.
Alisema ni mara nyingi wamekuwa wakiitaka kampuni hiyo
kuondoka ndani ya TTCL bila mafanikio jambo ambalo ni kuifanya TTCL
ishindwe kujiendesha.
Alisema tangu Bhart Airtel ipewe mkataba wa ubia ndani ya
TTCL wa umiliki wa wa hisa asilimia 35 imeshindwa kuwekeza na
kuiboresha kampuni hiyo kama walivyokubaliana hivyo kusababisha TTCL
kujiendesha kwa hasara.
"Kitendo cha Bhart Airtel kuendelea kumiliki hisa zake
hizo katika Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) ni sawa na kitendo cha
kuihujumu TTCL, na kuwa toka mwaka 2012 Celtel walitoa taarifa ya awali
ya kujiondoa ndani ya TTCL, na kuanzisha majadiliano ya uvunjaji wa
mkataba baina ya pande zote mbili" alisema Ndaro
Ndaro aliongeza kuwa hadi sasa majadiliano hayo yamekuwa
yakicheleweshwa na mwenye hisa ndogo pasipo kuwepo kwa sababu za msingi,
kitendo hiki ni sawa na hujuma, mmiliki mdogo mwenye hisa anatambua
kuwa TTCL haiwezi kupata mtaji mahali popote pasipo idhini yake.
Alisema Tewuta inapongeza juhudi zinazofanywa na Rais
Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali kwa kuwaunga mkono
kufuatilia jambo hilo na kuhakikisha wabia hao wanaondolewa ndani ya
TTCL.
Ndaro ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuungana
katika jitihada za kuwaondoa wabia hao Bhart Airtel ambao wanaihujuma
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
0 maoni:
Post a Comment