MAHAKAMA
ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 120 watu wanne akiwemo
aliyekuwa askari wa jeshi la Polisi baada ya kukutwa na hatia ya
unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, James
Mhanusi,ambapo mbali na kuwatia hatiani washitakiwa hao Mahakama hiyo
pia imemuachia huru mshtakiwa mmoja kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna
ushahidi unaomhusisha na tukio moja kwa moja.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali,Catherine Paul, aliwataja washtakiwa kuwa ni
aliyekuwa Askari wa Jeshi la Polisi,8303 Pc James, Elinazi Mshana,Lusajo
Jeremia na Abdalah Mohamed ambao kwa pamoja walitenda kosa la
unyang’anyi wa kutumia silaha Oktoba 7, 2013.
Mwendesha
mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 23/2014 walitenda
kosa hilo kinyume cha kifungu cha 287 (a) cha kanuni ya adhabu sura ya
16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo walifanikiwa kupora Kahawa
yenye thamani ya shilingi Milioni 119.2 yenye uzito wa kilogramu 30091.
Akisoma
Hukumu kwa watuhumiwa hao, Hakimu Mhanusi amesema kutokana na ushahidi
wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi mahakama imeona mshtakiwa
namba tatu katika kesi hiyo ambaye ni Gwantwa Malakasuka hakukuwa na
ushahidi unaomtia hatiani pasipo shaka hivyo akaamuru kuachiwa huru.
0 maoni:
Post a Comment