http://m.voaswahili.com http://m.voaswahili.com/a/2789267.html /a/278926MWANZO ENZI: Xavi atangaza rasmi 2789267 kuiacha Barca, mastaa watoa ushuhuda SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING Posted Mei23 2015 saa 11:32 AM IN SUMMARY Juzi Alhamisi, Xavi 35, alitangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa Barcelona ilikuwa imempa mkataba lakini akadai kwamba huu ulikuwa muda mwafaka kwake kuondoka katika klabu hiyo ambayo ameichezea tangu akiwa mtoto. SHARE THIS STORY 0 inShare CATALUNYA, HISPANIA MWISHO wa zama. Mwisho wa enzi. Kwa majonzi, kiungo mkongwe wa Barcelona, Xavi Hernandez ametangaza kuachana rasmi na klabu hiyo baada ya miaka 17 ya kucheza hapo na atakwenda kukipiga Al Sadd ya Qatar. Juzi Alhamisi, Xavi 35, alitangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa Barcelona ilikuwa imempa mkataba lakini akadai kwamba huu ulikuwa muda mwafaka kwake kuondoka katika klabu hiyo ambayo ameichezea tangu akiwa mtoto. Mechi yake ya mwisho ya La Liga itakuwa leo Jumamosi dhidi ya Deportivo, kisha atacheza katika fainali za Kombe la Mfalme dhidi ya Athletic Bilbao halafu atacheza katika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus Juni 6. “Ni uamuzi sahihi, siyo rahisi sana, ni muda mwafaka wa kuondoka. Bado najiona nina matumizi sana hapa, lakini kubadilisha mazingira ni muhimu. Kichwa changu kinaniambia hivyo, ingawa moyo wangu hausemi hivyo,” alisema Xavi ambaye alidai lengo lake ni kumaliza masomo ya ukocha na kurudi Barcelona. Aongoza mataji Hispania Xavi alisainiwa na shule ya soka ya Barcelona mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 11. Tangu hapo ametwaa mataji 23 katika misimu 17 aliyocheza. Mpaka sasa amelingana kimataji na mkongwe wa Real Madrid, Francesco Gento ambaye pia ana mataji 23. Kama akitwaa taji la Kombe la Mfalme dhidi ya Atletic, kisha akatwaa taji la Ulaya dhidi ya Juventus, Xavi atakuwa mchezaji mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya Hispania. Xavi vilevile ameichezea timu ya Taifa ya Hispania mechi133. Mastaa wafichua ya moyoni Lionel Messi: “Ilikuwa raha sana kucheza na Xavi. Ni mchezaji anayefanya mambo yaonekane kuwa rahisi sana. Anaziona pasi ambazo ni yeye mwenyewe tu anayeziona.” Sir Alex Ferguson (baada ya fainali za Ulaya 2009): “Messi hakuwa tatizo katika mechi hii. Tatizo lilikuwa kwa Iniesta na Xavi. Wangeweza kukaa na mpira usiku mzima.” Pep Guardiola: “Xavi ni mchezaji mwenye vipimo vya damu ya Barcelona. Ana ladha na mpira. Mchezaji ambaye amebaki kuwa mpole na ni mzalendo na mwaminifu kwa klabu.” 1 | 2 Next Page» Zilizosomwa Sana Yanga kauzu Kiberenge Mbeya City chatua Simba Vifaa vitatu kuziba pengo la Kaseke Moshi: Mpeni Cannavaro miaka minne ‘Nidhamu imempoteza Boban’ Kamara ni jembe Simba yampandia dau beki wa Yanga SC Mkude: Siingilii usajili, lakini Ivo habari nzito Bocco na kampeni kali Heh! Yanga mmezidi Xavi atangaza rasmi kuiacha Barca, mastaa watoa ushuhuda Habari Mpya Kiungo mpya Yanga mkwara Wachezaji Taifa Stars nao wajitathmini wenyewe ‘Nidhamu imempoteza Boban’ Moshi: Mpeni Cannavaro miaka minne Kiberenge Mbeya City chatua Simba Vifaa vitatu kuziba pengo la Kaseke Yanga kauzu Bocco na kampeni kali Xavi atangaza rasmi kuiacha Barca, mastaa watoa ushuhuda Mkude: Siingilii usajili, lakini Ivo habari nzito About us Contact us Kusudio Katao Emails RSS
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment