Breaking newssssssss; WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHITIKIZA BANDARI MAOFISA TRA KUSAKWA WATIMULIWE

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa  wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Habari kamili inaandaliwa. Fanya subira….
Kwa sasa anza na picha….
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.

 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa 
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.


from Blogger http://ift.tt/1kWNSik
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment