MAHAKAMA ZA ARDHI ZA KATA ZIJIREKEBISHE NA KUFANYA KAZI YAKE

MABARAZA ya adrhi ya kata yanadaiwa kuwa ni chanzo cha
migogoro ya ardhi badaya ya kuwa ndio kimbilio na usuruhishi wa migogoro hiyo
licha lengo la kuundwa kuwa ni utatuzi wa migogoro.
Hayo yanakuja baada ya baadhi ya wananchi akiwemo Prosper
Mgaya, kuona mabaraza hayo hayana msaada kwao kutokana na utendaji kazi wake na
kuona kuwa yamekuwa na rushwa nyingi na kuomba serikali kuyatengea fedha ili kuto
penda hongo kutoka kwa wanaotaka hudumia.
Alisema kuwa mabaraza hayo yamekuwa yakiongeza migogoro
badaya ya kupunguza na kuonekana ni bora kwenda mahakamani kuliko kwenda katika
mabaraza hayo.
Uundwaji wa mabaraza hayo inahitaji kuwa na watu wasio pungua
wanne na wasio zidi wanane na kuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume
na kutoa ruhusa ya mjume kutuma mwakilishi ila tu kwa wakili kuto mpa ruhusa ya
kutuma mwakilishi wakati wa kusikiliza mashauri.
Aidha waliiomba mamlaka husika kuteua wajumbe wenye elimu ya
sheria katika mabaraza hayo ili wasikilize mashauri ya ardhi kwa ufanisi mkubwa
badala ya ubabaishaji unaofanywa na wajumbe wasiokuwa na uelewa wa sheria.
Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo, aliahidi
kushughulikia muundo wa mabaraza hayo kupitia madiwani kwa jimbo hilo ili yawe
na ufanisi kwa jamii.
Alisema kuwa atahakikisha huwa mabaraza hayo yanakuwa msaada
kama ilivyo tarajiwa na madhumuni ya kuundwa kwake.
“Kupitia madiwani wa kata za jimbo hili watayapitia mabaraza
haya na kuyaunda upya ili kuondoa vitendo vinavyo waletea shida wananchi na
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki,” alisema Mwalongo
Mabaraza ya aridhi yameundwa hapa nchini chini ya sheria ya
ardhi namba 2 ya mwaka 2002 kifungu cha 10 cha sheria hiyo pia inaelezea muundo
wa mabaraza hayo pamoja na uwezo wake, mabaraza hayo yapo katika kila wilaya na
yanauwezo wa kusuruhisha migogoro ya ardhi na mabaraza hayo yanatakiwa kutumia
sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na ile ya ardhi ya vijiji ya mwaka huohuo.
  

from Blogger http://ift.tt/1TfUfrP
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment