JUNI KUZIMA SIMU ZA KICHINA HAPA NCHINI

Upo hapo? TCRA imesema 40% ya simu zinazotumika nchini ni feki na kufikia mwezi wa sita mwezi huu zote hazitaweza tumika kwa mawasiliano nchini.

Katika semina spesheli iliyoandaliwa jana (3/02/2016), afisa wa mawasiliano wa shirika hilo, Bwana Innocent Mungy alielezea data hizo. Kupitia kifaa spesheli kinachofahamika kwa jina la Central Equipment Identification Register (CEIR) TCRA wataweza kutambua simu zote zisizo na sifa za kutumika.

Tarehe 16 mwezi wa sita ndio mwisho wa simu zisizo na sifa kuweza kutumika kwa mawasiliano.

Ukiacha simu zingine zinazokuja na majina yasiyoelewa simu nyingi feki huwa zinaiga hadi muonekano wa matoleo maarufu ya simu za iPhone na Samsung Ni simu gani hazitakuwa na sifa?

Simu feki…..
Hizi ni simu zinazotengenezwa na viwanda bubu hasa hasa nyingi zinaingia kutoka nchini Uchina. Simu hizi saa nyingine zinaiga muonekano ata wa makampuni makubwa yanayofahamika duniani kwa sifa za ubora, mfano za Samsung au Apple – lakini mnunuaji akizichunguza vizuri anakuta ni feki.

Simu za wizi…
Wizi wa simu janja unazidi kukua duniani kote
Hii ni sifa nyingine kwa simu zitakazowezwa kuzuiliwa kutumika. Pale ambapo mtu ataibiwa simu na kutoa ripoti polisi na huku akiipa polisi namba ya IMEI ya simu husika basi namba hiyo itawekwa kwenye mashine hiyo spesheli na kuhakikisha simu hiyo haitaweza kupata huduma za mawasiliano nchini. Yaani mwizi akiweka laini yeyote ya simu atashindwa kuitumia.

Hali itakuwaje?
Kuna uwezekano wa takribani mamilioni ya simu zinazotumiwa kwa sasa na wananchi mbalimbali nchini hasa wa hali ya chini kuathirika na zoezi hili. Tayari TCRA inawataka watu wafanya zoezi la kuthibitisha kama simu wanazotumia ni feki au la, ili kama ni feki basi waanze kutafuta utaratibu mwingine wa kununua simu nyingine.

Kuna faida yeyote ya uamuzi huu wa TCRA?
Ndio kwa kiasi kikubwa. Kuna maumivu kwa wengi hasa wa hali ya chini kutokana na kulazimishwa kutafuta simu nyingine ili hali lilikuwa jukumu la serikali kuhakikisha simu feki, zisizo na ubora kutoingia nchini – tatizo lishatokea sasa tuganje yajayo…na katika ilo faida zipo.

Faida kuu ni kwamba watumiaji watakuwa salama zaidi kwa kutumia bidhaa zenye sifa na ubora wa kimataifa na si simu zenye ubora mbovu zinazowaweka katika hatari – kiusalama na kiafya.

Pia kwa sasa simu tunazitumia kwa mambo mengi hii ikiwa ni zaidi ya kupiga na kupokea simu… uamuzi huu utahakikisha huduma za kibenki za simu zinakuwa salama. Unapokuwa na simu isiyo na viwango vya usalama wa kimataifa unakuwa katika hatari ya data zako kudukuliwa na wadokozi wa kimtandao.

Mwaka 2012 Kenya pia walifanya uamuzi kama utakaofanywa na TCRA mwezi wa sita, na takribani watu milioni 1.5 waliathirika na kutoweza kutumia simu zao tena kwa mawasiliano.

from Blogger http://ift.tt/1mjwUKK
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment