Mh. Edward Mwalongo Kwanza kusoto na Mwasona Emmanuel wakiwa mahakamani Jana wakati sesi yao ikiwa tayari kwa kutajwa |
MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imetoa siku nne kwa walalamikiwa kumpamajibu wakili wa upande wa mashitaka katika kesi ya kupinga matokeo ya mwaka 2016 iliyoanza kusikilizwa jana mkoani Njombe.
Amri hiyo inakuja baada ya wakili wa mshitaki Emmanuel Masonga aliye kuwa mbombe Ubunge Jombo la Njombe (Chadema) katika kesi ya kupinga matokeo Edwin Swale baada ya kuomba mahakama isiendelee na kesi kabla hajajibiwa na upande unao lalamikowa.
Mbele ya Jaji Jacob Mwambegele Swale walisema kuwa anaomba kujibiwa majibu yake kutoka kwa wakili wa serikali Apmarck Mabruck ambaye alisimama kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Eluminata Mwenda.
Swale aliomba majibu baada ya kuomba kujibiwa malalamiko yao kutoka kwa washitakiwa katika shitaka hilo ambapo akupata majibu hayo ambayo yalitakiwa ayapate ili kuenmdelea na kesi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza na ilikuwa mahakamani hapo kwaajili ya kutajwa.
Jaji Mwambegele aliiahirisha kesi hiyo kwa kutoa amri kwa wakili wa serikali kuhakikisha nakala ya majibu inamfikia wakili Swale ndani ya siku nne na ili ayapitie majibu hayo na kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo itatajwa tena.
Swale ambaye anasimama mahakamani kumuwakilisha Masonga ambao wanapinga matokeo katika mahakama kuu kanda ya Iringa wanawashitaki watu watatu katika kesi hiyo ya uchaguzi ya mwaka 2016.
Watu wanao shitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wajimbo la Njombe kusini Edward Mwalongo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurigenzi wa mji wa Njombe Eluminata Mwenda na mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda ambaye ndio alikuwa mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe.
Kesi hiyo aliyo beba hisia za wakazi wa mji wa Njombe waliofurika mahakamani kujua nini kinaendelea imeahirishwa na Jaji Mwambegele ambapo itasomwa tena Februari 25 mwaka huu.
Hata Wakili msomi Swale baada ya kesi hiyo kuahilishw akatika mahakama ya mkoa wa Njombe ambapo mahakama kuu imeendesha kesi zake hapo aliwataka wakazi wa mkoa wa Njombe kuendelea kufuatilia keshi hiyo na kuendelea kujitokeza kwa wingi kila siku ya kesi.
from Blogger http://ift.tt/1oZSEgW
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment