Agizo hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe na mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatory Choya, wakati akizindua wiki ya unywaji wa maziwa kitaifa ambayo inaadhimishwa mkoani Njombe kitaifa wakati kukiwa na asilimia 52 ya udumavu mkoani humo.
Alisema kuwa mkoa wa Njombe ndio unaonoza kwa kufuga ngombe wanaotoa maziwa kwa wingi lakini wakazi wake hawanywi maziwa.
“Mkoa wa njombe una ng’ombewa maziwa wapatao 15,412 ambao huzalisha 8,696,440 ambapo kwa wastwastania kila wana Njombe anakuywa robo lita kwa siku huu ni mwanzo mzuri lakini ipo ya ya kuongeza nguvu ya uzalishaji,” alisema Choya.
Ameongeza kuwa serikali kama itataka kila shule kuwa na maziwa halmashauri hazita weza kifedha basi zianzishe miradi ya ufugaji wa ng’ombe mashuleni.
Katika maadhimisho hayo Ofisa mifugo mkuu Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Abdallah Temba alisema selikali inasambaza madume Bora ya Ng’ombe ya Mbegu ili kuwasaidia wafugaji kupata Ng’ombe wa Mbegu kwa urahisi.
“Serikari kwa kushirikiana na wadau inahakikisha kuwa inazalusha ng’ombe bora wa maziwahasa madume yenye historia yakutoa maziwa mengi ambayo yatamsaidia mfugaji kufuga kwa tija,” alisema Temba.
Hata hivyo katika maadhimisho hayo wadau mbalimbali wa maziwa wameweka mabanda yaokatika uwanja wa maonyesho ya wiki moja ambapo kutatolea elimu juu ya ufugaji bora na wananchi kujionea bidhaa za maziwa.
Mbali na hayo, Zena Issa Ofisa Viwango wa Shirika la Viwango Nchini TBS alisema wameshiriki maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa jamii ili kutumia bidhaa zilizo sindikwa na kuthibitishwa na shiriki la viwango na kuwataka wananvhi kuhakikisha wanakuwa mbali na bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
Alisema kuwa kwa bidhaavza maziwa ambazo hazijasibitishwa zinakuwa hazina nembo ya TBS na wananchi wawe wachunguzi ili kupata vitu bora.
“Ukiona bidhaa za kampuni moja zingine zina arama ya ubora na zinine hazina basi ujuembazo hazina bado hazijakidhi viwango vya ubura,” alisema Issa.
Hata hivyo afisa masoko wa TBS Debora Haule, alisema kuwa kupitia maonyesho hayo wasindikaji wanakaribishwa katika banda lao ili kujua taratibu za kuthibitisha bidhaa zao kabla hawajaziingiza sokoni
from Blogger http://ift.tt/27XtilT
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment