JOTO LA BAHARINI LASABABISHA BARIDI NA MVUA NDOGONDOGO NJOMBE

MAMLAKA ya hali ya hewa Tanzania mkoa wa Njombe imesema kuwa mvua na baridi kali iliyopo katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini inatokata na kuongezeka kwa joto kwenye bahari ya hindi.
Meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Njombe, Michael Abushiri alisema kuwa kwa mujibu wa utabili wa hali ya hewa wa siku kumi baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini kutakuw ana hali ya mvua na mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Abushiri akizungumza na Elimtaa Blog mkoani Njombe amesema kuwa hali hii imekuwa hivi kwa mwaka huu tofauti kidogo na mwaka jana ni kutokana na ongezeko la joto baharini.
“Joto la bahari ndilo linalo sababisha hii hali ya hewa mnayo iona kwa kuwa sasa majira yamebadirika kutokana na shughuli za kibinadamu na kwa mkoa wa njombe kutokana na hali ya ke ya ubaridi kukiwa na hali ya unyevuvyevu baridi huongezeka tofauti na maeneo mengine ya joto ambako kukiwa na unyevu huwa na joto” alisema Abushiri.
Aidha kutokana na hali ya hewa kuwa hivyo mamlaka hiyo inatoa hadhari kwa wakulima kuvuna mazao yao mapema kama mahidi yasije haribika kutokana na Mvua.
Hali ya hewa hiyo imesababisha baridi kali kwa maeneo ya Njombe mjini na jamii yake ikiwa imejisitiri kwa nguo nzito na mvua za rasharasa zikidondoka asubuhi, huku vipindi vya jua kikiwa kwa muda mfupi mchana.
Kwa wakuliama wanao andaa mashamba mamlaka inasema hali ya hewa hii haita kuwa na madhara kwa shughuli za uandaaji wa mashamba yao.
“Hali hii ya mvua ndogondogo hazina madhara kwa wale wanao fanya maandalizi ya mashamba yao kwa kuwa mvua hizi ni za mda mfupi tu na tahadhari hii tumeitoa katika vyo mbo vya habari lakini wananchi wamekuwa wavivu wa kufuatilia utabili wa hali ya hewa,” Aliongeza Abushuri. 
Michael Abushiri meneja hali ya hewa Mkoa wa Njombe
Mcichael Abushiri meneja mamlaka ya hali ya hewa Tanzania mkoa wa Njombe

from Blogger http://ift.tt/2b1g3Yv
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment