Watu 12 wafariki dunia papo hapo, miili yatabuliwa, Rais atuma salamu za lambilambi

WATU 12 wamepoteza maisha na watu zaidi ya 10 kujeruhiwa katika ajali ya basi mali ya kampuni ya New Forse yenye nambari za usajili T 429 DEU iliyotokea juzi usiku majira ya saa 1:15 ikitokea Jijiji Dar Es salaam kulekea mkoani Ruruma.

Katikaajali hiyoiliyo gharimu maisha wa watu 10 wakubw ana watoto wawili inadaiwa kuwa chanzochake ni mwendo kasi ambapo kabla ya kuacha njia ilianza kutembelea tairi za upande mmoja na kupinduka zaidi ya mara tatu na kupondeka vibaya.

Akizungumza katika eneo la tukiomda mfupi baada ya kumalizashughuli zauokozi lilizotumia zaidi ya masaa 5 kamanda wa polisi mkoa wa njombe Prudensiana Protas alisema kuwa ajali hilo imeondoa uhai wa watu 12 huku kati yao mwili mmojaumeelekea mkoani songea na miili 11 ikiwa imehifadhiwa katika Hopitali ya Kibena ya mkoa wa Njombe.

Alisema kuwa majina ya marehemu bado hayajatambuliwa na kuwa watu walio safirija ndugu na jamaa kwa siku ya jana kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, na Njombe wawasiliane na ndugu zao ili kujua kama wamefika salamana kama hawapatikani wafuatilie ili kuzitambua maiti hizo.

Alisema kuwa kuwa chanzocha ajali hiyo ni mwendokasi wadereva wagari hiyo ambaye jina lake halijafahamika mara moja na kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili kumpata dereva hiyo ambaye alikimbilia kusiko julikana mara baada ya ajali hiyo.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe Joseph Mwasabeja alisema kuwa shughuli ya uokoaji ilikuw ani nzito na kuchukua mda mrefu mpaka kukamilika kwake ni kutokana na gari hiyo kuharibika vibaya.

Alisema kuwa ni zaidi ya masaa matano waliyo yatukia kuondoa miili ya marehemu na majeruhi walio kuwa wamekwama katikagari hiyo iliyo pondeka vibaya.

“Ajali hii ni maya kuwahi kutokea miili mingi ilikuwa imekwama ndani na ilibidi tuitoe kwa ustadi wa hali ya juu ili kuto iharibu zaidi na majeruhi kuto waumiza zaidi,” alisema Mwasabeja.

“Hata hivyo kikosi chetu tunakabiliwa na changamotoya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi lakini kwa muda tulifikakwa muda muafaka na kuanza kazi maramoja,” aliongeza.

Majeruhi na mashuhuda wa ajali hiyowanasemakuwa gari hiyoilikuwa katika mwendomkali na kuwa kabla ya kupinduka zaidi ya mara mbili na kuserereka ilimshinda dereva zaidi ya mara tatu na hatimaye ilitembelea magurudumu ya upande mmoja na kupinduka.

Pascal Mkombwe alisema kuwa gari hiyoilimshinda rereva kilimota moja kabla ya eneo ambali ilitokea ajali kuwa kuwa alihama upande wake na kurejea akahama mara ya pili na kutrejea kisha gari hiyo ikapinduka baada ya kutembea kwa magurudumu ya upande wa kushoto na kujikita katika shimodogo la pembeni mwa barabara.

“Mimi nilikuwa nimefunga mkanda gari ilianza kumshinda dereva katika kona ya kwanza akaiweza baada ya muda kidogo ikamshinda tena akaiweza ilipo mshida mara ya mwisho ni katika kona hii ya tano ambapo gari ilitembea kwa tairi za upande mmoja kisha ikapindika,” alisema Mkombwe.

Haya hivyo Marko Mgaya aliemakuwa ilipo mshinga mara ya kwanza dereva alikaa kimya lakini mara ya mwisho alisikia Sauti ya dereva akisema ‘aya’ ndipo akasikia kishindo kikubwa.

 Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi jana aliwasilisha salamu za lambilambi zilizotumwa na rais Dr John Magufuli, alisema kuwa serikali ipo pamoja na wafiwa, na anawaombea majeeuhi wapone mapema.

Dr Nchimbi amesema kuwa ndugu wa marehemu kuwa wadulivu wakati wa kipindi hiki kigumu.

Aidha kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Kibena mkoani Njombe, Dr Francis alisema kuwa Miili yote iliyokuwa imehifadhiwa katika hospitali hiyo imetambuliwa na ndugu, na juchukuliwa kwaajili ya mazishi.

Amesema kuwa miili hiyo imesafirishwa jana kwenda Songea, Dar es salaam na Zanzibar.

Alisema kuwa katika hospitali hiyo majeruhi wanaenderea vizuri.

from Blogger http://ift.tt/2d12Q4N
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment