Rais atuma salamu za rambirami, majina ya marehemu yatambulika

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuri, amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Njombe kufuatia ajali ya New Force ambapo miili yote ya waliofariki katika ajali hiyo wamesafirishwa kwenda wa ndugu zao.

Salamu hizo za Rais  zimesomwa na Mkuu wa mkoa wakati miili ya marehemu ikichukuliwa katika chumba cha kuhifadha maitu ambapo miili yote imechukuliwa huku mingine ilirudi Dar es Salaam na mingine ikienda Zanzibar.

Mkuu wa mkoa wa njombe alisema kuwa rais anawaombia wafiwa hao kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindihiki kigumu huku majeruhi wakiombewa kupona haraka.

Mkuu wa mkoa wa Njombe alitoa onyo kwa madereva ambao wanakuwa na mwendokasi wakati polisi maeneo hayo hawapo na kuwataka kuto endeshwa na polisi wa usalama barabarani.

Alisema “Haiwezekani madereva wakawa wanaendesha mwendo wa kasi wakifika maeneo ambayo hakuna polisi, tunataarifa kuwa kila mkiondoka songea mnakuwa na mwendo mkali kabla ya kufika mjini Njombe na mnapo enda Songea mkifika Kifanya mwendo wenu unakuwa mbaya,” aliongeza Dr Rehema.

Mkuu wa mkoa wa Njombe aliongoza kuwa wahanga wa ajali hiyo ambao walifika katika Chumba cha kuhifadhia maiti kuchukua miili ya maiti ambapo imesafirishwa kwenda sehemu mbalimbali ambako marehemu hao wametarajiwa kuzikwa jana.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali Kibena, Dr. Francis Benedict, alisema kuwa miili tisa imesafirishwa kuelekea mkoani Ruvuma na miili miwili imesafirishwa kuelekea Jijiji Dar es salaam huku mwili mmoja ukisafirishwa kwenda Zanzibar katika mkoa wa Kuzini Unguja.

Aidha alisema kuwa hali ya majeruhi katika hospitali hiyo inaendelea vizuri huku wengine wakuruhusiwa, ambapo alisema kuwa wanaume ni wawili na wanawake ni wanne waliosalia kupatiwa matibabu hospitalini hapo huku ndugu wa majeruhi waliosalia katika hospitali hiyo wakiwa na taarifa.

Dr Benedick anawataja marehemu hao kuwa ni Beteina Mhenga, mkazi wa Songea, Prottesa Mwingira mkazi wa Preramiho, Maria Mapunga, (4) Peramiho,  Salma Njovu, (50) Dar Es salaam, Pets Ngonyani wa Dar es Salaam (8).

Aliwataja wengine kuwa ni Angela Juate Morres (25) Kusini Unguja, Reuben Matembo (45), Dar es salaam, Hellena Chale (25) Songea, Hossana Mbuesa (20) Songea, Nurdini Mpunga Songea, na mmoja hakufahamika jina.

Ajali ya basi za kampuni hiyo ya New Force iliyo tokea Septemba 19 mkoani Njombe ni ya tatu kutomea mkoani humu katika maeneo tofauti huku ajali hiyo iliwa ndio inaongoza kwa vifo vingi.

from Blogger http://ift.tt/2d3TrfQ
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment