WANANCHI wa kijiji cha Idindilimunyo kata ya Igwachanya
Wilaya ya Wangingo’mbe Mkoa wa Njombe walifanya maandamano baada ya
mwalimu kuhamishwa na mkurugenzi bila kuwapo kwa sababu za kumuhamisha.
Wakizungumza na Nipashe baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walisema
walishindwa kuelewa sababu zilizo tumika na Mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kumuhamisha mwalimu huyo pasipo kuwaletea mwalimu mwingine wa kuziba
nafasi
hiyo.
Tatizo hilo la walimu katika shule hiyo ya Idindilimunyo inauhaba wa walimu
ambao wamestaafu mwaka jana nakufanya tatizo kubwa la walimu katika shule
hiyo.
Aidha wanachi hao wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Gorden
Kasanga waliulaumu uongozi wa kata ya igwachanya kuwa huenda walikula njama
ya kumhamisha mwalimu huyo kupitia Mwenyekiti wa halmashauri .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
wanging’ombe Mohamed Kasinge aliwaonya wananchi hao kuwa wamekiuka
kanuni na sheria zilizo wekwa na serikali juu ya maandamano
kwani wanaweza kusababisha matatizo makubwa.
Kisinge alisema walipaswa kujadili kwanza kabla hawajanza maandamano hayo
katika ofisi ya uongozi wa kata ya Igwachanya ili waweze kusikilizwa.
Hivyo Kisinge alisema uwepo walimu saba katika shule hiyo hakuwezi athiri taaluma
katika shule hiyo huku akisema kunabaadhi ya shule nyingine zina walimu watatu
lakini kiwango cha taaluma kipo juu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wangingo’mbe Amina Kiwanuka amewataka wananchi
kuyaweka kwenye mawazo yao ya kuhitaji Walimu ili halmashauri iweze
kushugulikia tatizo hilo ,Alisema maandamo yamekiuka
sheria na kanuni za maandamano.
from Blogger http://ift.tt/2b6pSoj
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment