BIDHA ZISIZO FAA ZA MABILIONI ZATEKETEZWA

BIDHAA zilizo kwisha muda wake zenye thamani ya zaidi ya milioni 7 na zile ambazo hazijasajiliwa kutumika hapa nchini zimeteketezwa mkoani Njombe baada ya kufanyika msako wa duka kwa duka na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini.

Mkaguzi wa mamlaka hiyo kanda ya nyanda za juu Kusini, Dr. syrivester Mwidunda, akizungumza baada ya zoezi la uteketezaji, alisema kuwa malmaka hiyo imekuwa ikifanya ugaguzi wa kawaida katika maduka mbalimbali ili kubaini bidhaa ambazo hazijasajiliwa kutumika hapa nchini.

Alisema kuwa katika ukaguzi wao huwa wamekuwa pia wakiangalia bidhaa aambazo zina viambata sumu ambapo pia hutazamwa na zile zilizo kusha muda wake ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wanatumia bidhaa bora zisizo na madhara kiafya.

Alisema kuwa wakiwa na ukaguzi huo mkoa wa njombe katika wilaya zake zote wamebaini kuwapo kwa didhaa zenye uzito wa kilo 882 zenye thamani ya shilingi milioni 7.4 (7,447,000) ambazo ni vinywaji, vipodozi na bidhaa ambazo muda wake wa matumizi umekwisha.

Hata hivyo wito umetolewa kwa jamii ya watanzania kuhakikisha kuwa wanakuwa makini wanapo nunua bidhaa madukani na kuangalia muda wa kuisha matumizi yake (Expire date) ili kuto tumia vitu hivyo huku wakihakikisha kuwa hawatumii mafuta ya kupaka yenye viambata sumu.

Aidha mratibu wa TFDA mkoa wa Njombe Inosensia Mtega alisema kwa magonjwa ya kasa sasa yamekuwa mengi ni kutokana na matumizi ya bidhaa hizo ambazo muda wa matumizi yake umekwisha na wale wanao tumia vipodozi vyenye viambata sumu.

Alisema kuwa madhara ya matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu huwa ni baada ya muda mrefu na kuwa baada ya hapo mtu huugua Kansa.

Alisema kuwa ni rahisi kuacha matumizi ya vipodozi kuliko kutibu kansa ambayo matibabu yake ni kukata kiungo ama kuchomwa na mionzi ambako ni gharama na hatimaye ni kifo.

Mtega amesema kuwa baada ya kutolewa sana elimu sasa wauzaji wa vipodozi na watumiaji wamepungua tofauti na miaka ya hapo nyuma ambapo watumiaji walikuwa ni wengi na katika maduka vipodozo vilikuwa vikipatikana kwa wingi.

from Blogger http://ift.tt/2dDSzOd
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment