Wananchi waamua kujenga Barabara yao wenyewe


BAADHI ya wananchi wa mitaa wa Kambarage na Nzengelendete Halmashauri ya Mji wa Njombe
 Mbunge Mhe. Lucia Mlowe akifanya mahojiano na Elimtaa Media katika Ujenzi huo
 Baadhi ya wakazi wakifanya ukarabati
Mhe. Lusia Mlowe mbunge mkoa wa Njombe Viti maalumu akusambaza kifusi
Na +255 753321191 Njombe

wameanza kujihami na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kwa kuanza kujaza vifusi katika barabara inayo ingia katika mitaa hiyo kutoka barabara kuu ya Songea – Njombe.


Wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona kuwa kikifika kipindi cha Mvua barabara hiyo haipitiki na ukarabati unakuwa ni mgumu kufanyika huku mara nyingi hurazimiaka kukatika uwanja wa ndege.

Wakizungumza huku wakiendelea na shughuri za ujenzi wa barabara hiyo wananchi hao walisema kuwa ni heri kujihami kwa kudhibiti mashimo mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha na kujiondoa na adha ya kujifunga barabara yao.

Semeni Msigwa alisema kuwa kipindi cha mvua wamekuwa wakiacha matumizi ya magari yao kwa kuyaacha mali na makazi yao kwa kukwepa kunasa katika tope kitu kilicho wasukuma kuwnza kujaza kifusi katika maeneo ya mashimo ya barabara.

Msigwa alisema kuwa kama wakifanikiwa kumaliza barabara yote kujaza kifusi adha inayo wakuta mara kwa mara wakati wa mvua msimu wa mvua zijazo watapita kwa raha.

Adha hiyo haiishii kwa watumiaji wa vyombo vya moto pekee Nikolaus Mkongwa anasema kuwa wamekuwa pia watembea kwa miguu wakipata shida ya kutumia barabara hiyo na kuomba serikali kufanya utaratibu wa kutenga bajeti kwaajili ya ukarabati wa kudumu kwa kuweka changalawe barabara hiyo.

Alisema kuwa kutokana na barabara hiyo kuwa ni tya vumbi kipindi cha mvua hugeuka kuwa tope na kuwalazimu kakatisha katika katrika uwanja wa Ndege wa mkoa wa njombe na kuzua mgogoro na walizi wa uwanja huo.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Njombe Mhe. Lucia Mlowe anaungana na wananchi hao kusambaza Kifusi katika eneo hilo ili suala alilolishuhudia msimu uliopita la kutasa kwa magari ya wakazi wa mtaa huo na huduma za kijamii kusimama.

Akiwa eneo hilo alisema kuwa ameamua kujiunga na wananchi hao ili matukio hayo kuto jirudua na kwa kuwa bajeti ya mwaka huu haijatengwa maalumu kwa ajili ya eneo hilo.

Alisema kuwa kujaza kifusi hicho na kushindiliwa mapema kunaweza kuwa suruhisho la matatizo ya kujifunga kwa barabara hiyo na kuwa saidia wananchi kuitumia barabara hiyo msimu wote.

from Blogger http://ift.tt/2d7SSCr
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment