ASKARI Polisi mwenye cheo cha Koplo, Evarist Furaha wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani amekufa kwa kujipiga risasi




ASKARI Polisi mwenye cheo cha Koplo, Evarist Furaha wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani amekufa kwa kujipiga risasi kwa bahati mbaya wakati akielekea kwenye lindo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Blasius Chatanda ameyasema hayo kwa waandishi wa habari alipokuwa akitolea ufafanuzi tukio hilo.

Chatanda amesema ajali hiyo ilitokea Novemba 28, mwaka huu saa moja usiku, Maili Moja eneo la Sokoni, Kata ya Maili moja.


Amesema, Furaha aliingia kazini jioni katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kibaha na alikuwa amepangiwa lindo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment