Chiku Abwao amevunjiwa mkataba wa upangaji katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Iringa




ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu kwa nyakati tofauti mkoani Iringa kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chiku Abwao amevunjiwa mkataba wa upangaji katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Iringa, baada ya kutuhumiwa kukiuka masharti ya upangaji.

Abwao alikuwa mpangaji wa jengo lenye klabu maarufu ya VIP lililopo Plot Na 36 katika Mtaa wa Haile Sellasie, Kata ya Gangilonga, mjini Iringa; na kinyume cha masharti ya mkataba, akapangisha jengo hilo kwa mtu mwingine aliyetajwa kwa jina la Alex Mgeta na kujipatia mamilioni ya shilingi.

Novemba 28 asubuhi, Abwao alijaribu kudhibiti mkataba wake kwa kufunga makufuli yake juu ya makufuli ya klabu hiyo, hatua iliyosababisha uongozi wa klabu hiyo kutoa taarifa Polisi na NHC kabla ya kuchukua hatua za kuvunja makufuli hayo.

Pamoja na kufunga jengo hilo, Abwao aliweka ulinzi kwa kutumia kampuni binafsi ya ulinzi ili wahusika wasivunje makufuli hayo na kuingia ndani, akidai biashara ni yake na katika jengo hilo kuna mali zake nyingi zikiwemo kreti za bia, soda, viti na meza.
Ukiwa na uongozi wa NHC, saa nane mchana, uongozi wa klabu hiyo ulivunja makufuli hayo, ukaifungua klabu na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Kaimu Meneja wa NHC Mkoa wa Iringa, Lepson Usia alisema shirika lao limevunja mkataba na Abwao baada ya kubaini amevunja baadhi ya masharti ya upangaji.
Usia alisema ni kosa kwa mujibu wa taratibu za shirika hilo kumpangisha mtu mwingine na akatoa mwito kwa wapangaji wao kutofanya kosa hilo kwani wakibainika watachukuliwa hatua kama iliyochukuliwa kwa Abwao.

Awali Msimamizi wa Club VIP, Leonard Lukasola amesema waliingia mkataba wa siri wa upangaji wa jengo hilo na Chiku Abwao kwa muda wa miaka mitatu.

 Alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo, Abwao alisema hajawahi kuwa na mkataba wa ubia wa kibiashara na mpangaji aliyepewa mkataba mpya na NHC, bali alikuwa akifanya naye kazi kama promota wa biashara zake katika jengo hilo linalotumiwa pia na wasanii wa muziki kutoa burudani.

Kuhusu kujipatia mamilioni ya shilingi baada ya kumpangisha mpangaji mwingine, Abwao alisema fedha alizokuwa akilipwa na promota huyo hazikuwa za kodi pekee yake, kwani zilihusisha na mapato yatokanayo na biashara na faida yao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment