BABA wa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Xavery Mizengo Pinda (90) amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,


BABA wa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Xavery Mizengo Pinda (90) amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, alikokuwa akitibiwa.
Tangazo lililotolewa jana na Mwandishi wa Waziri Mkuu, Irene Bwire, lilieleza kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Pinda, anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mzee Xavery Pinda alifariki jana saa 9:30 alasiri hospitalini hapo.


Kutokana na kifo hicho, Pinda katika tangazo hilo aliwataarifu ndugu walioko katika kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi, walioko nje, viongozi wa serikali na chama tawala na vyama vingine vya siasa kuhusu msiba huo.

Tangazo lilieleza kuwa taratibu za maziko zinafanyika nyumbani kwa Pinda, Zuzu, mkoani dodoma na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment