Joyce Kapesa anayedaiwa kuwa mwalimu hewa kwa zaidi ya miaka 13, amekimbia kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi miwili sasa




MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kamawe iliyoko katika Kata ya Sundu, wilayani Kalambo mkoani Rukwa, Joyce Kapesa anayedaiwa kuwa mwalimu hewa kwa zaidi ya miaka 13, amekimbia kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi miwili sasa akihofia kukamatwa na kushtakiwa.

Ofisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, John Maholani amekiri kuwa mtumishi huyo hayupo kwenye kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi miwili kwa hofu ya kuwa mwalimu ‘hewa’ kwa zaidi ya miaka 13.

Amesema mwalimu huyo aliajiriwa kwa mara ya kwanza Juni 2003 kama mwalimu wa kawaida kisha akapandishwa cheo na kuwa Mwalimu Mkuu katika Shule ya Msingi Mikonko kwa miaka minne na Shule ya Msingi Kamawe kwa zaidi ya miaka miwili.

Amefafanua kuwa, madiwani wa halmashauri hiyo watapoketi katika kikao chao cha Baraza la Madiwani, watatoa uamuzi wa mwalimu mkuu huyo “hewa” mtoro pamoja na watumishi wengine ambao wamebainika kutumia vyeti feki wakiwa watumishi wa umma.

Diwani wa Kata ya Sundu, Peter Simuyemba amedai kuwa, mwalimu huyo aliripoti katika Shule ya Msingi Kamawe kama Mwalimu Mkuu miaka miwili iliyopita.

Amesema Oktoba 6, mwaka huu mwalimu huyo aliandika barua kwa Mwalimu Msaidizi wa shule hiyo, akiomba ruksa ili akawahudumie wazazi wake ambao alidai ni wagonjwa.

Kwa mujibu wa Simuyemba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Sundu (ODC), Kapesa siku hiyo alimkabidhi Mratibu wa Elimu wa Kata hiyo barua ya kuacha kazi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment