Leo
November 30 2016 msajili wa hazina, Lawrance Mafuru amekutana na
waaandishi wa habari, pamoja na mambo mengine suala aliloligusia ni
pamoja na benki nyingi nchini kulalamika kufilisika wakati huu ambapo
serikali imeamua fedha zake kuziweka benki kuu na kuzitoa katika mabenki
ya biashara.
Mafuru
ameeleza kuwa kufilisika kwa mabenki ni kutokana na kukopesha zaidi ya
trilioni 1.4 kwa watu huku madeni hayo kutokuwa na uhakika wa kulipwa na
sio pesa za serikali zilizopo benki kuu kwa sasa.
>>>’Mpaka mwezi
september sekta ya mabenki imekopesha zaidi ya trilioni 17, hiyo ni
mikopo ambayo watanzania, sekta za umma wamekopa, kwenye mikopo hiyo 9%
au trilioni 1.43 ni mikopo mibovu maana yake kuna watu wamekopa pesa
hazijarudi’
0 maoni:
Post a Comment