Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimelaani shambulizi la kigaidi lililotokea katika soko la mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Umoja wa Ulaya pia imelaani hujuma hiyo iliyoua raia kadhaa mjini Mogadishu na kutangaza azma yake ya kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kudhamini usalama wa taifa hilo la Pembe ya Afrika.
Mripuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari uliotokea Jumamosi iliyopita katika lango la kuingilia soko la mji mkuu wa Somalia, Mogadishu uliua zaidi ya raia 10 wengi wao wakiwa wanawake. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo, ingawa kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab limehusishwa na jinai hiyo.
0 maoni:
Post a Comment