Kauli yake inakaribisha mjadala mwingine mrefu na ambao ni ngumu kupata mshindi kuhusu iwapo anachofanya Darassa sasa ni hip hop!
Kupitia Instagram, Afande ameandika:
Mtu yeyote anaetumia AKILI katika jambo lake mara nyingi hufikia malengo…wapo madogo zangu wengi wakali sana…mimi wote nawakubali lakini umuhimu wa kipekee nampa @darassacmg ‘El Classico Darasa’ leo hii ni kwa sababu kaja kukanusha uzushi na upuuzi wa kuiaminisha jamii kwamba hiphop imekufa kiasi cha wengine kuthubutu kuinajis hiphop kwa kuilinganisha na singeli…Roho saba katika moja ya mistari yake ndani ya wimbo Nakupenda hiphop anasema’Hiphop ndio mziki na hili lake biti…Amba nipe kiki niwabastie mamluki….Nakupenda Hiphop…Nakuheshimu @darassacmg ….Here we go bro….Darassa amekuwa kwenye headlines tangu aachie wimbo wake Muziki unaoaminika kuwa ndio wimbo namba 1 Tanzania kwa sasa.
0 maoni:
Post a Comment