Paa la kanisa katika mjini uliopo kusini mashariki mwa Nigeria,
limeanguka na kusababisha vifo vya takriban watu 60. Idadi ya watu
waliopoteza maisha inahofiwa kuongezeka.
Kanisa hilo la kiinjilisti la Reigners Bible Ministry kwenye mji wa
Uyo katika jimbo la Ibom, lilikuwa limefurika waumini baada ya paa
ambalo bado linaendelea kujengwa lilipoanguka Jumamosi hii.
Miili ya takriban wahanga 60 imeondolewa tayari.
Gavana Udom Emmanuel aliripotiwa kuwemo ndani ya kanisa hilo baada ya paa hilo lenye vyuma lilipoanguka japo hakujeruhiwa.
“We have never had such a shocking incident in the history of our dear state,” Emmanuel aliandika kwenye ukurasa wa Facebook.
Rais Muhammadu Buhari ametuma salamu za rambirambi. Shirika la habari
la serikali limedai kuwa kati ya watu 50 – 200 wanaweza kuwa wamepoteza
maisha.
September 2014, watu 115 people wakiwemo 84 raia wa Afrika Kusini
walipoteza maisha mjini Lagos baada ya kanisa la mchungaji maarufu TB
Joshua kuanguka.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment