Mamia wamuaga mpiga picha Mpoki Bukuku



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameongoza mamia ya waandishi wa habari na wakazi wa jiji la Dar es salaam, kumuaga mpiga picha wa magazeti ya The Guardian Limited, Mpoki Bukuku
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe (Kulia) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea (Kushoto)
aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita .

Bukuku alifariki dunia saa chache baada ya kugongwa na gari katika eneo la ITV Mwenge Wilayani ya Kinondoni wakati akitoka kazini.

Wengine waliomuaga marehemu ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, na Mbunge wa Ubungo, Mh. Saed Kubenea ambaye aliwakilisha Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari, MOAT.

Akizungumza msibani, Mh. Nape amesema, tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia taaluma ya habari na kuwataka waandishi wa habari kuiga kazi nzuri zilizofanywa na marehemu Mpoki enzi za uhai wake.

Kwa upande wake, Mh. Mbowe amemuelezea marehemu Bukuku kama mpambanaji aliyefanya kazi yake kwa weledi mkubwa.
Mwili wa marehemu umesafirishwa leo saa kumi jioni kuelekea Dodoma ambapo maziko yatafanyika kesho.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment