Goodluck Gozbert ni miongoni mwa waimbaji wa muziki wa Gospel kutoka nchini Tanzania ambao wanafanya vyema katika Tasnia ya muziki wa Injili na siku ya tarehe 25 Dec 2016 alifanya tamasha lake katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ambalo lilihudhuliwa na wakazi wengi kutoka mbeya na mikoa mingine ya jirani.

Tamasha hilo lilisindikizwa na Baadhi ya waimbaji kutoka Dar na Mbeya, ambapo kutoka Mbeya tamasha lilipambwa na Martha Baraka, Josephat Mwanjisi, Happy Kamili na Yakobo Mwamboya na kutoka jijini Dar es salam tamasha lilipambwa na Neema Mudosa, Aniset Butati na Mess Chengula.
JICHOPEMBUZI  imekuletea baadhi ya picha za matukio yaliyotokea siku hiyo ambayo ilikuwa ni ya baraka na neema kwa wakazi wa mkoani Mbeya. Karibu
Muimbaji Goodluck Gozbert akiwahudumia wakazi wa Mbeya.
Muimbaji Goodluck Gozbert akiwaonyesha upendo wapenzi wake.
Muimbaji Neema Mudosa naye pia aliwahudumia wakazi wa Mbeya.
Muimbaji Happy Kamili naye pia alihudumu vyema siku ya tamasha hilo.
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria katika tamasha hilo hapa wakiwa katika furaha ya kubarikiwa.
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria katika tamasha hilo hapa wakiwa wanaselfika huku wakiendelea kubarikiwa.
Goodluck Gozbert akiendelea na huduma.





Mess Chengula naye hakuwa nyuma alihudumu vyema siku hiyo.