Baada ya kutolipwa mishahara yake kwa miezi minne, mchezaji Venance Joseph Ludovic wa klabu ya Mbao FC ya mkoani Mwanza ameomba kuvunja mkataba na klabu hiyo.
Barua iliyoandikwa tarehe 13.12.2016 yenye kichwa kichwa kinachosomeka: NOTISI YA KUVUNJA MKABA NA TIMU YA MBAO FC, inaeleza madai ya mchezaji Ludovic huku notisi hiyo ikiwa ni ya saa 24 akitaka kulipwa pesa zake za mishahara pamoja na pesa za usajili.
Badua hiyo imeelekezwa kwa Katibu Mkuu wa Mbao FC lakini Ludovic amepeleka nakala ya barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa TFF na SPUTANZA kwa taarifa.
0 maoni:
Post a Comment