Watengezaji
wakubwa wa simu za mkononi TECNO Mobile na Klabu ya ligi ya Uingereza,
Manchester City wamesherehekea uzinduzi wa ushirikiano wa kimataifa kwa
miaka kadha kama mshirika rasmi wa Klabu ya mpira ya Manchester City.
TECNO Mobile itashirikiana na klabu hiyo kukuza mikakati ya masoko na
matangazo ya kampeni sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo bara la Afrika
ambapo TECNO tayari inatambulika kama kinara wa soko la simu za mkononi.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa
ushirikiano huo wa kimataifa uliofanyika kwenye kituo cha mafunzo na
uangalizi wa maendeleo ya vijana, Afisa Mkuu wa Biashara wa City Football Group Tom Glick amesema …>>>“Tunafurahi
kuwakaribisha TECNO Mobile katika mkusanyiko wa ushirikiano wa
kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko ya nyumbani kunaendana na
namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia kushirikiana nao
kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote”
Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile Stephen Ha alizungumza katika uzinduzi huo wa kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha Manchester City kwamba
>>>“Tunashukuru
sana kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana ya
Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa muda mrefu katika michezo
kwa hali ya juu kwa kuwapatia wateja wetu uzoefu wakufurahia zaidi simu
bora isiyolinganishwa na nyingine”
0 maoni:
Post a Comment