Nape: Tutawaachia kidogo wasanii, hatutobana sana
Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema amesikia kilio cha wasanii kuhusu kuwabana katika kazi zao hususan kwenye video za muziki na kuahidi kufumba jicho moja ili kuwapa uhuru kiasi.
Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye tuzo za EATV zilizotolewa kwa mara ya kwanza Jumamosi hii kwenye ukumbi wa Mlimani City.
“Tutaachia kidogo hatutabana sana, “alisema Nape. “Na mimi nimepita mtaani naambiwa ‘Nape mmebana sana.’ Wakati mwingine tunataka kufanya mambo tunaambiwa tumepitiliza. Wakati mwingine tutafumba jicho moja watu wapitilize kidogo ili mambo yaende sawa sawa,” alisisitiza waziri huyo aliyekuwa mgeni rasmi kwenye tuzo hizo.
Kwa muda mrefu Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA lililo chini ya wizara yake, limekuwa likilaumiwa kwa kutoa adhabu kali kwa wasanii kwa kile inachosema ni kuvunja maadili.
0 maoni:
Post a Comment