Watanzania waaswa kutumia bidhaa za ndani ya nchi



sidotraining-makingfruitjamWatanzania wameaswa kutodharau bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi na kukimbilia bidhaa za nje ya nchi. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameyasema hayo leo, alipotembea banda la Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) katika maonyesho ya viwanda vya Tanzaniaa yanayoendele Uwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere (Saba Saba), Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania haitaweza kuwa nchi ya viwanda ikiwa watanzania wenyewe hawathamini bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi. “Ili tufanikiwe katika uchumi wa viwanda lazima tuanze kwa kile tunachoweza kwa kutumia rasilimali tulizonazo ndani ya nchi,” alifanunua Dkt. Mpango.
Aliendelea kwa kusema kuwa, watanzania wengi wanadharau mashine ambazo zinatengenezwa na SIDO ambazo gharama yake ni nafuu ukilinganisha na mashine zinazotengenezwa nje ya nchi. Vile vile amesema kuwa haiwezekani hata jembe la mkono liagizwe toka nje ya nchi wakati kuna viwanda ndani ya nchi ambavyo vinauwezo wa kutengeneza majembe yenye ubora.

Aidha ameishauri SIDO kutengeneza mashine nyingi na kusambaza nchi nzima ili watanzani waweze kujiajiri na hata kufungua viwanda vidogo vidogo kwa kutumia mashine hizo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin Rutageruka amesema kwamba maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa ni endelevu ambapo yatakuwa yakifanyika kila mwaka mwezi Desemba yakiambatana na maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Ameeleza kuwa, lengo la monyesho hayo ni kubadilishana uzoefu na kutoa fursa katika sekta ya viwanda, kutoa hamasa kwa watanzania kununua bidhaa za ndani ya nchi, kuunganisha wazalishaji na wenye malighafi, kuwawezesha watafiti na wabunifu kuonana na wenye viwanda, kutoa fursa kwa watanzania kujua palipo na viwanda pamoja na kuwawezesha vijana na wanafunzi kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha viwanda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment