Noti ya 500 kuendelea kutumika- BOT



Benki Kuu ya Tanzania imekanusha taarifa zinazozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijami kwamba noti za shilingi mia tano hazitatumika tena kuanzia Desemba 31, 2016 na kusema kuwa taarifa hizo siyo taarifa za kweli ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Noti ya shilingi mia tano.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki (BOT), Marcian Kobello amesema kuwa ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment