Sijutii kabisa kuacha ualimu- Timbulo



Msanii Timbulo ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usisahau' amefunguka na kusema toka ameacha kufundisha na kuachana na fani yake ya ualimu na kukimbilia kwenye muziki
Msanii Timbulo
hajawahi kujutia maamuzi hayo kwani muziki umekuwa ukimpa mafanikio makubwa zaidi.
Timbulo alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo ya EATV na kusema saizi hakuna kitu kingine anachofanya zaidi ya muziki na kila kitu unachomuona nacho au anachomiliki ni kutokana na kazi yake hiyo ya muziki.

"Kwa kiasi kikubwa nafanya muziki wenye faida, niliacha kazi ya ualimu na kufanya muziki hivyo sijutii kabisaa kuacha ualimu kwani toka nimeingia kwenye muziki sijawahi kufanya kazi nyingine na kila kitu unachoniona nacho sasa au nachomiliki sasa ni kutokana na kazi yangu ya muziki na kama ningeendelea kuwa mwalimu nisingekuwa namiliki vitu nilivyonavyo sasa" alisema Timbulo 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment