Wajasiriamali Coco Beach wangoja mamilioni ya Rais



Idadi kubwa ya wateja wanaokwenda kupata huduma na mahitaji katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, imetajwa kuwa moja ya vigezo vinavyowafanya wafanyabiashara katika eneo hilo kuwa kundi la mwanzo linalostahili kunufaika na uwezeshaji wa
milioni hamsini zilizopangwa kutolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa vijiji na makundi ya wajasiriamali nchini.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo na wafanyabiashara hao kupitia kwa msemaji wao Bw. Bernard Mwinuka maarufu kama Mpoto, ambaye amesema ongezeko hilo la wateja linatokana na ufahamu walionao Watanzania wa kupenda kutumia vitu vya asili tena vile vinavyolimwa na kutengenezwa nchini kwao.

Bw. Mwinuka amemuomba Rais Magufuli kuelekeza nguvu zake kwao na wafanyabiashara wengine kama wao, ambao amesema tayari wameanza kutumia malighafi za kilimo kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuziongezea thamani huku wakitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment