
Timu ya Dar es Salaam Young Africans leo December 2 2016 imeingia mkataba na serikali kwa ajili ya kupewa kibali cha kutumia uwanja wa Taifa na Uhuru kwa mechi zake za kitaifa na kimataifa.
Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesaini mkataba huo kuiwakilisha Yanga huku upande wa serikali ukiwakilishwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel.
Moja kati ya masharti waliyopewa Yanga
katika mkataba huo ili waweze kupata kibali cha kuutumia uwanja huo,
kama ikitokea uharibifu wowote utakaofanywa na mashabiki au wachezaji wa
Yanga, timu hiyo itaingia gharama za kulipia matengenezo.
0 maoni:
Post a Comment