Director Ajez Bale awataka Waimbaji wa Muziki wa Injili Tanzania wajiandae kabla ya kufanya Video zao.


Muandaaji na Mtayarishaji wa Video hapa Nchini Director Adam Mwaibale maarufu kama Ajez Bale amewaomba waimbaji wa muziki wa Injili kujiandaa wanapotaka kufanya Video zao ili kupunguza kasoro katika video zao.

Akizungumza na Gospo Media katika Kipindi cha Excullusive Interview kinachorushwa na Gospo Tv alisema kuwa waimbaji wengi wa gospel wanashindwa kufanya maandalizi yao vizuri ndio maana wanaharibu video zao.

Waimbaji wa muziki wa Injili wajiandae na watulie pindi wanapotaka kufanya video zilizopo kwenye kiwango kuliko kukurupa tu,ndio maana unakuta mwimbaji wimbo wake unaitaji wachezaji yeye anakuwa hajawaandaa sasa hapo anakuwa anampa kazi Director kuanza kutafuta watu wakucheza na hapo unakuta mwimbaji anakwambia anataka kazi yake ndani ya wiki moja au mbili sasa hapo unafikiri utafanya kazi gani kwa mfano.

na wengine wanashangaza kwakweli unakuta mwimbaji hata wimbo wake hajaukariri unakuta una kazi kubwa wakati wa kuedit kazi maana midomo inapishana yaani ni kazi kwelikweli ninachoweza kuwaomba waimbaji wajitahidi kufanya maandali mazuri kabla ya kuanza kutafuta Director wa kufanya kazi yake mimi niko tayari kufanya kazi  na mwimbaji yoyote mkubwa kwa mdogo ili kazi itoke vizuri na katika viwango vya hari ya juu.”Alisema Director Ajez Bale

Director Ajez Bale amekwisha kufanya kazi za waimbaji mbalimbali na kazi zao zinafanya vyema vituo mbalimbali vya media  hapa nchini ikiwemo kazi ya Sababisho ya Baraka Mwampamba na Robert Mdemwa pamoja na kazi ya Siku Zinakuja ya Jacob Sanke na kwasasa yupo katika katika maandalizi ya kumalizia kazi ya Mwimbaji anayefanya vizuri kwasasa Daudi Mpemba na wimbo wake Mnyang”anye shetani
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment