Leo tumekuwekea vipaji vitano ambavyo vilikuwa ni moto wa kuotea mbali ndani ya Kenya,Kama ifuatavyo..
1. DJ Sadic
Sadic anafahamika sana kwa uchezaji santuri (DJ)na pia ni host wa kipindi cha tukuza kinachoruka katika runinga ya KTN kila jumapili. Mchezaji santuri huyu (DJ )alileta mtazamo mpya alipotoa kibao kipya kwa jina holy ghost party ,wimbo huu wake ulipata umaarufu haswa miongoni mwa vijana nchini Kenya.
2.Producer Majic Mike
Producer Majic Mike amekuwa producer kwa muda sasa lakini kile wengi walikuwa hawamfahamu mpaka pale wimbo wake wa Ayaya ambao aliimba mwenyewe kuingia kwenye tuzo za Groove na wimbo wake wa Light It Up kushinda tuzo za Xtreem.
3. Sammy Dee
kila unapo taja Sammy Dee ,wengi humtambua na kazi ya ubunifu wa video ,kitu ambacho wengi hawajatambua ni kuwa Sammy Dee alikuwa mmoja wa kundi la Bmf na mwaka huu alirejea kwenye muziki kwa kutoa kibao chake kinachoitwa Overflow
4. Dj Ruff
Baada ya kunyakua tuzo ya groove kama DJ bora wa mwaka Ruff amezidi kutamba haswa baada ya kuangusha kibao chake na Danny Gift pamoja na J Fam kinachofahamika kama La La La.
5. DJ Tabz
DJ Tabz ni moja ya Ma DJ maarufu nchini Kenya na kwa mwaka 2016 alitamba sana baada ya kushirikishwa kama mwimbaji kwenye wimbo wa Give Thanks
0 maoni:
Post a Comment