Kijana anayedai kufanana kimuonekano na msanii wa bongo fleva Harmonize kutoka WCB, ameibuka na kushusha lawama akidai kuwa msanii huyo alimnyanyapaa pale alipotaka kuzungumza naye na kujimbulisha kwake.
Harmo Rapa
Kijana huyo ambaye anajulikana kwa jina la Harmo Rapa, amejitambulisha mbele ya kamera ya eNewz ya EATV kuwa Rapa na ana ndoto za kufanya makubwa katika muziki lakini anahitahitaji mtu wa kumshika mkono mkono.
Harmo Rapa amesema anaamini anafanana na Harmonize na kwamba amekuwa akifananishwa sana na msanii huyo.
Msikilize mwenye hapa akifunguka kupitia eNewz