Kampuni za simu nchini kufutiwa leseni




Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetishia kusitisha kwa muda au kufuta kabisa leseni ya biashara kwa kampuni zote za mawasiliano nchini, zitakazoshindwa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba
Hatua hiyo ni kulingana na sheria mpya ya fedha ambayo imetoa ukomo wa hadi Desemba 31 mwaka jana kampuni hizo ziwe zimejisajili katika soko hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam hii leo; Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema kwa sasa wanasubiri maelezo kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana  (CMSA) kuhusu idadi ya kampuni za mawasiliano zilizokidhi sifa za kusajiliwa katika soko la hisa kwa ajili ya kuchukua hatua kwa zile zilizokaidi kutekeleza agizo hilo la kisheria.

Mhandisi Kilaba amesema TCRA imeikabidhi CMSA orodha ya kampuni zaidi ya 80 za mawasiliano, orodha ambayo CMSA itaipitia kwa lengo la kuchuja na kupata kampuni ambazo zinastahili kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kauli ya Mhandisi Kilaba imekuja huku taarifa kutoka soko la Hisa la Dar es Salaam zikionesha kuwa ni kampuni tatu pekee ndizo zimejisajili katika soko hilo, licha ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo wake Jumamosi ya Desemba 31 mwaka jana.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment