Waziri wa kilimo
wa Rwanda Geraldine Mukeshimana ametoa wito kwa wafanyabiashara
wanaoagiza bidhaa za mifugo kutoka Uganda na nchi za Ulaya kuacha
kuagiza kwa muda bidhaa zote za mifugo kutoka Uganda na nchi za Ulaya
kutokana na mlipuko wa homa ya mafua ya ndege katika maeneo hayo.
Waziri huyo
amewataka wafugaji wote kufungia mifugo yao ili kuepuka mwingiliano kati
yao na ndege wasiofugwa, na kwamba watu wanatakiwa kukaa mbali na ndege
pori ambao watakutwa wamekufa, na kutoa taarifa haraka kwa mamlaka
husika.
Uganda
imethibitisha kuwa mlipuko wa ugonjwa huo unaambukiza kwa ndege, ambao
pia unaweza kuwapata binadamu. Wizara ya kilimo ya Uganda imesema ndege
waliopatwa na ugonjwa huo mpaka sasa ni ndege aina ya Membe, bata na
kuku.
0 maoni:
Post a Comment